CHRISC
Arusha youth league ni mashindano yanayo andaliwa na CHRISC kila mwaka. Chrisc
ina matawi manne ambayo ni Tanga, Mwanza, Manyara, Kilimajaro, na Arusha ambapo
ndipo makao makuu ya CHRISC Tanzania.
CHRISC
ARUSHA YOUTH LEAGUE FINAL 2012
Final
ya ligi ya CHRISC Arusha kwa mwaka huu kama kawaida ya kila mwaka ilifanyika
katika zone moja iliyo jumuisha washindi wa zone zote za CHRISC Arusha. Final
hii ilifanyika katika kituo cha Eso almaarufu kama kituo cha Palot ambacho hufanya shughuli za kaendesha league ya CHRISC. Timu zilizo fuzu kucheza final ya league ya
CHRISC kwa mwaka huu ni pamoja na Tacoda fc kutoka kituo cha kaloleni ambacho
kinaendesha ligi katika kiwanja cha Soweto. Yosso united pia kutoka kaloleni
under 16, paloti under16 na14 pia kutoka kituo cha Esso, na hardroock kutoka
kituo cha Suye na Kijenge youth na Tiger
Boys kutoka kitio cha Suye
FINAL
CHRISC
Arusha kwa mwaka huu kwa final ilianza tarehe 17/11/2012 kwa robo final
iliyozikutanisha team kutoka zone zote katika kituo cha Suye. Na team zilizo
fuzu final ndizo zilizoshiriki fainal kitika kituo cha Esso. Michezo ya fainali
ilianza majira ya saa 3 kamili kwa michezo ya under 12 na mshindi wa umri hii
alitoka katika kituo cha Suye kwa team ya Kijenge youth. Baada ya apo ilichezwa
fainali ya under 14 iliyo chezwa kati ya team ya Tacoda fc na team kutoka
katiki kituo cha Meserani na Tacoda fc waliibuka washindi wa umri huu. Pia
baada ya apo ilichezwa mechi ya under 16 iliyozikutanisha team za Hardroock na
palot na hatimaye Palot waliibuka washindi wa umri huu. Pia baada ya hapo
ilichezwa mechi ya under 17 iliyokutanisha team za Yosso united na Tiger Boys
ya kutoka Suye na mshindi wa mechi hii alikua ni timu ya Tiger Boys.
No comments:
Post a Comment