Thursday, December 15, 2011

BONANZA LA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

15-12-2011
Witten by; Paul Edward Jr na Steven Minja
Photos; Paul Edward Jr

BONANZA LA SIKU YA UKIMWI DUNIANI LILIFANYIKA SIKU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI NA LILIHUSIHA MICHEZO MBALIMBALI KAMA MPIRA WA MIGUU MPIRA WA WAVU NA KIKING EIDS OUT

Maandamano.
Tanzania Maandamano yalianza saa 04;00 asubuhi kuzunguka eneo la suye Arusha kuanzia kiwanjani na kumalizikia kiwanjani.yalihusisha timu zote zilizo shiriki bonanza. Pamoja na viongozi wote dhumuni la maandamano haya madogo ni kuielimisha jamii kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi waandamanaji wote waliimba bila ukimwi inawezekana.Bonyeza picha



Mpira wa miguu.
Timu zote za wasichana na wavvulana zilizo shiriki bonanza zilijiandaa vizuri na kucheza kwa ushindandani wa hali ya juu. Bonanza lilishirikisha timu kutoka vituo vyote vinne kulikua na jumla ya mechi nane. Kila timu ilicheza jumla ya mechi tatu na matokeo mshindi wa kwanza alikua kaloleni zone, wapili suye na watatu ngaramtoni. Wasichana walikua wa kituo cha meserani na suye na bingwa alikua meserani alisinda goli 1-0.

Mpira wa wavu.
Maandalizi mazuri yalifanyika kwa timu zote zilizo shiriki mpira wa wavu. Kulikua na jumla ya timu 2 kutoka kituo cha suye kimandolu mshindi alikua ni mana.


ATHARI ZA UKIMWI

Ugonjwa huu una athari kubwa na nyingi katika jamii yetu,zifuatazo ni baadhi ya athari za ukimwi katika jamii yetu,
· KUWA NA FAMILIA YATIMA,
· UMASKINI,
· KUKOSA WATAALAM,
· UZALISHAJI DUNI,
· KUKOSA VIONGOZI BORA,

Na athari nyingine nyingi.

Elimu hii ndiyo iliyo tolewa katika siku ya maadhimisho ya ukimwi duniani pia elimu hii iliambatana na michezo mbalimbali ikijumuisha jinsia zote,Michezo hiyo ilkua ni
Mpira wa miguu kwa jinsia zote,Mpira wa wavu kwa wavulana,Michezo ya kuelimisha(caw games).
Na baada ya kumaliza michezo wa chezaji wote walipatiwa chakula.

Imeandaliwa na,
Paul.edward45@yahoo.com
Posted by Picasa