Thursday, May 17, 2012

CULTURE WORKSHOP


17/05/2012

Written by: Chrisc Tanzania media team
Photos by: Chrisc Tanzania media team

SEMINA YA UTAMADUNI

Semina hii iliendeshwa na CHRISC Tanzania kupitia mradi wa CHRISC TRAINING CENTRE ARUSHA[CTCA].Mradi huu upo katika shule ya msingi Suye. Semina hii ilianza tarehe kumi na tisa hadi tarehe ishirini mwezi wa nne 2012 pia semina hii ilikuwa na washiriki kumi na nne kutoka katika eneo la Suye.Semina hii iliongozwa na mwalimu wakikundi cha sanaa.Mwalimu huyu anaitwa Abubakary Amin












MALENGO YA SEMINA HII
Dhumuni kubwa au lengo la semina hii ni kuwa na kikundi kikubwa cha sanaa na maigizo  ambacho kitakuwa chini ya CHRISC TRAINING CENTRE ARUSHA[CTCA], kikundi hiki kitakuwa kikifanya mambo yafuatayo kuimba,kuigiza na sarakasi. Pia kuna maono ya kukitumia katika mashindano makubwa ya EAST AFRICA CUP yanayofanyika Moshi ambayo CHRISC ni mmoja wa waandalizi.

MAFUNZO KWA VITENDO












Semina hii ilikuwa na vipindi viwili vikubwa ambavyo ni mafunzo ya darasani na vitendo[natharia] kulikuwa na mafunzo ya kuimba na kuigiza.Pia baada ya kumalizika kwa semina hii wameendelea na mazoezi  ya kila siku katika shule ya msingi Suye.Tunawakaribisha wale wote wenye vipaji vya kuigiza na kuimba.