CHRISC
ARUSHA YOUTH LEAGUE FINAL 2012
FINAL
CHRISC
Arusha kwa mwaka huu kwa final ilianza tarehe 17/11/2012 kwa robo final
iliyozikutanisha team kutoka zone zote katika kituo cha Suye. Na team zilizo
fuzu final ndizo zilizoshiriki fainal kitika kituo cha Esso. Michezo ya fainali
ilianza majira ya saa 3 kamili kwa michezo ya under 12 na mshindi wa umri hii
alitoka katika kituo cha Suye kwa team ya Kijenge youth. Baada ya apo ilichezwa
fainali ya under 14 iliyo chezwa kati ya team ya Tacoda fc na team kutoka
katiki kituo cha Meserani na Tacoda fc waliibuka washindi wa umri huu. Pia
baada ya apo ilichezwa mechi ya under 16 iliyozikutanisha team za Hardroock na
palot na hatimaye Palot waliibuka washindi wa umri huu. Pia baada ya hapo
ilichezwa mechi ya under 17 iliyokutanisha team za Yosso united na Tiger Boys
ya kutoka Suye na mshindi wa mechi hii alikua ni timu ya Tiger Boys.