17/05/2012
Written by: Chrisc
Tanzania media team
Photos by: Chrisc
Tanzania media team
SEMINA YA UTAMADUNI
Semina hii iliendeshwa na CHRISC Tanzania kupitia mradi wa
CHRISC TRAINING CENTRE ARUSHA[CTCA].Mradi huu upo katika shule ya msingi Suye.
Semina hii ilianza tarehe kumi na tisa hadi tarehe ishirini mwezi wa nne 2012
pia semina hii ilikuwa na washiriki kumi na nne kutoka katika eneo la
Suye.Semina hii iliongozwa na mwalimu wakikundi cha sanaa.Mwalimu huyu anaitwa
Abubakary Amin
MALENGO YA SEMINA HII
Dhumuni kubwa au lengo la semina hii ni kuwa na kikundi
kikubwa cha sanaa na maigizo ambacho
kitakuwa chini ya CHRISC TRAINING CENTRE ARUSHA[CTCA], kikundi hiki kitakuwa
kikifanya mambo yafuatayo kuimba,kuigiza na sarakasi. Pia kuna maono ya
kukitumia katika mashindano makubwa ya EAST AFRICA CUP yanayofanyika Moshi
ambayo CHRISC ni mmoja wa waandalizi.
MAFUNZO KWA VITENDO
Semina hii ilikuwa na vipindi viwili vikubwa ambavyo ni
mafunzo ya darasani na vitendo[natharia] kulikuwa na mafunzo ya kuimba na
kuigiza.Pia baada ya kumalizika kwa semina hii wameendelea na mazoezi ya kila siku katika shule ya msingi
Suye.Tunawakaribisha wale wote wenye vipaji vya kuigiza na kuimba.